

Lugha Nyingine
Wilaya ya Shexian ya Mkoa wa Anhui yahimiza kuhifadhi mabaki ya kale ya kitamaduni na kujenga upya hali ya miji (2)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 23, 2025
SHEXIAN – Wilaya ya Shexian mkoani Anhui, mashariki mwa China iko kwenye sehemu ambayo Milima Huangshan inapakana na Mto Xin'an. Wilaya hiyo imepata kiini cha utamaduni na majengo ya mtindo wa Huizhou. Mji wa Kale wa Huizhou, ulioko katikati ya wilaya hiyo ya Shexian, ni moja ya miji ya kale iliyohifadhiwa vizuri zaidi nchini China. Mtandao wake wa mitaa, vichochoro, na madaraja ya kale unaendana vema na makazi ya kijadi, mahekalu ya mababu, na minara ya ukumbusho.
Katika miaka ya hivi karibuni, wilaya hiyo ya Shexian imekuwa ikihimiza kuhifadhi mabaki ya kale ya kiutamaduni na kujenga upya hali ya miji, ikivuta watalii kujichangamanisha katika mapatano kati ya mazingira ya asili na utamaduni ambao hufafanua mji huo wa kihistoria.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma