Wanahabari wa shughuli ya Mawasiliano ya Kirafiki ya Vijana ya BRI wafika Luoyang, China kutembelea Bustani ya Maua ya Peoni (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 22, 2025
Wanahabari wa shughuli ya Mawasiliano ya Kirafiki ya Vijana ya BRI wafika Luoyang, China kutembelea Bustani ya Maua ya Peoni
Maua ya Peoni yakiwa yamechanua kwenye Bustani ya Taifa ya Maua ya Peoni katika Mji wa Luoyang, Mkoa wa Henan, China. (Lu Yang/People’s Daily Online)

Jana Jumatatu, Tarehe 21, Aprili, waandishi wa habari 12 kutoka nchi 9 za Ulaya na Asia wanaoshiriki shughuli ya Mabadilishano ya Kirafiki ya Vijana ya "Ukanda Mmoja, Njia Mojia" (BRI) inayoandaliwa na People's Daily Online walifika kwenye Bustani ya Taifa ya Maua ya Peoni kujionea uzuri wa ustawi wa Enzi ya Tang ya China ya kale, kujaribu teknolojia ya kisasa ya bustani na kupata ufahamu wa kina wa upandaji maua ya Peoni na maendeleo ya utamaduni ya maua ya Peoni ya Luoyang.

Bustani hiyo ya Taifa ya Maua ya Peoni ya Luoyang nchini China ilijengwa kuanzia Mwaka 1984. Maua ya peoni zaidi ya laki 2 yamepandwa kwenye bustani hiyo, yakijumuisha spishi zote za maua ya peoni ya China na jeni kuu za aina za maua hayo ya peoni duniani. Ni jukwaa muhimu linalojumuisha utamaduni wa maua ya peoni, utafiti wa kisayansi, uthamini, na mawasiliano.

Katika kipindi cha siku 6 za kufanya mahojiano juu ya shughuli hiyo, waandishi hao wa habari pia watatembelea vivutio vingi mjini humo ili kujionea mafanikio mapya ya Luoyang katika kuhimiza ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na maendeleo ya uchumi wazi n.k.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha