Zimbabwe yaadhimisha miaka 45 tangu kupata uhuru (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 21, 2025
Zimbabwe yaadhimisha miaka 45 tangu kupata uhuru
Wanajeshi wa Zimbabwe wakitembea kwa ukakamavu kwenye gwaride la kijeshi kuadhimisha Siku ya Uhuru mjini Gokwe, Jimbo la Midlands, Zimbabwe, Aprili 18, 2025. (Xinhua)

HARARE - Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ameongoza wananchi wake katika kuadhimisha miaka 45 tangu nchi hiyo kupata uhuru katika jimbo la kati la Midlands, akitoa shukrani zake kwa ukombozi na juhudi zilizofanywa baada ya uhuru katika kuendeleza na kuifanya Zimbabwe kuwa ya kisasa.

Mvua ilishindwa kuzuia hali ya shamrashamra, kwani maelfu ya Wazimbabwe walimiminika Ijumaa katika ukumbi wa Gokwe kuadhimisha miaka 45 tangu nchi hiyo ijipatie uhuru, iliyotokana na gwaride la kijeshi.

Rais Mnangagwa alianza sherehe kuu kwa kushiriki katika desturi za muda mrefu za maadhimisho hayo, zikiwemo za kuwasha mwenge wa uhuru na kukagua gwaride la kijeshi.

Katika hotuba yake, Rais Mnangagwa amesema licha ya vikwazo vya nchi za Magharibi, matatizo yanayotokana na mabadiliko ya tabianchi, na misukosuko ya uchumi wa dunia, uchumi wa Zimbabwe unaendelea kuongezeka.

“Baada ya ukame wa mwaka jana uliosababishwa na El Nino, ambao ulidhoofisha ukuaji wa uchumi hadi asilimia 2, uchumi wa Zimbabwe unatarajiwa kukua kwa asilimia 5.6 mwaka 2025, chini kidogo kutoka makadirio ya awali ya asilimia 6, ikitokana na kuimarika kwa kilimo na madini,” Mnangagwa amesema.

Amesema Zimbabwe inatarajia mavuno mengi katika msimu wa majira ya joto wa 2024/2025, ambayo yanatarajiwa kuimarisha usalama wa chakula wa kaya.

Akitoa wito wa kuongezwa uwekezaji katika biashara za kilimo ili kufungua fursa kamili ya ardhi, Rais Mnangagwa amesisitiza haja ya kufanya kazi kwa bidii na juhudi za kila mara kuelekea kufikia ustawi wa kiuchumi na kujitosheleza.

"Kupitia juhudi zetu, hebu tubaki kuwa watu huru, wenye kujitegemea, na wenye mamlaka, ambao ni wamiliki wa hatma yetu wenyewe," amesema rais huyo.

Amesema serikali ya Zimbabwe inapigania kikamilifu mageuzi ya kilimo, maendeleo ya vijijini, na ustawi, na kujitahidi kwa ajili yakufikia dira ya nchi hiyo ya kuwa na uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2030.

“Umoja, amani na usalama ni mambo muhimu kwa maendeleo endelevu na ustawi nchini Zimbabwe,” amesema, akiongeza kuwa nchi hiyo inahimiza uvumbuzi, kuendeleza minyororo ya thamani ya kuvuka mipaka, na kuongeza fursa za ubia kati ya sekta ya umma na binafsi ili kuendesha ujenzi wa mambo ya kisasa na maendeleo ya viwanda ya nchi hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha