Shehena ya 7 ya msaada wa dharura wa kibinadamu kutoka China yawasili Myanmar iliyokumbwa na tetemeko la ardhi (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 21, 2025
Shehena ya 7 ya msaada wa dharura wa kibinadamu kutoka China yawasili Myanmar iliyokumbwa na tetemeko la ardhi
Shehena ya saba ya msaada wa dharura wa kibinadamu uliotolewa na serikali ya China ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Yangon nchini Myanmar, tarehe 20 Aprili 2025. (Xinhua/Myo Kyaw Soe)

YANGON – Shehena ya saba ya msaada wa dharura wa kibinadamu uliotolewa na serikali ya China imewasili jana Jumapili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Yangon, katika nchi ya Myanmar, iliyokumbwa na tetemeko kubwa la ardhi la 7.9 tarehe 28, mwezi Machi.

Vifaa hivyo vya msaada vikiwemo pamoja na maboksi 800,000 ya vidonge vya amoxicillin, chupa 122,000 za sindano za paracetamol na mannitol, mabokisi 225,000 ya vidonge vya cefradine, na chupa 480,000 za tembe za ibuprofen, ambavyo ni vyenye uzito wa tani 95.

Tetemeko hilo la ardhi vimesababisha vifo vya watu 3,726 na watu 5,105 kujeruhiwa, huku wengine 129 wakiwa hawajulikani waliko hadi kufikia Aprili 18, kwa mujibu wa takwimu rasmi za Myanmar.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha