Kupanda kwa halijoto kwaongeza shughuli za wakazi na matumizi mjini Chongqing, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 21, 2025
Kupanda kwa halijoto kwaongeza shughuli za wakazi na matumizi mjini Chongqing, China
Wakimbiaji wakivuka mstari wa kumalizia mbio kwenye mashindano ya mbio yaliyofanyika katika Eneo la Jiangbei la Mji wa Chongqing, kusini-magharibi mwa China Aprili 13, 2025. (Xinhua)

Wakiwa na shauku ya kujitoa kutoka kwenye maisha ya kukwama nyumbani wakati wa majira ya baridi kali, Wachina wanakumbatia shughuli za nje ya nyumba huku majira ya mchipuko yakitoa fursa zisizo na kikomo za kufanya mazoezi ya kujenga mwili na kufurahia uzuri wa mazingira ya asili.

Kadiri halijoto inavyozidi kupanda, mbio za marathoni, kuendesha baiskeli, kuvulia samaki kwa ndoano na kupiga kambi kumezifanya bustani za umma na maeneo ya biashara kuwa vituo motomoto vya shughuli mbalimbali, ikichochea wimbi kubwa la matumizi. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha