

Lugha Nyingine
Ndege kubwa inayoweza kutua kwenye maji ya China ya AG600 yapata cheti chake (4)
![]() |
Ndege kubwa nne za kuzima moto za AG600 zikionekana kwenye majaribio ya kuendeshwa mjini Pucheng, Mkoani Shaanxi, kaskazini magharibi mwa China, Desemba 2023. (Aviation Industry Corporation of China/kupitia Xinhua) |
BEIJING - Ndege kubwa ya zima moto inayoweza kutua kwenye maji ya AG600 iliyoundwa na China imepata cheti chake jana Jumapili kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya China (CAAC) mjini Beijing, ikionyesha mafanikio yake ya kuendelezwa na kuidhinishwa kuingia rasmi sokoni.
Ni hatua kubwa ya uwezo wa maendeleo wa China katika sekta ya ndege kubwa zenye madhumuni maalum na tasnia ya vviwanda vya kutengeneza ndege za kiraia, imesema kampuni iliyosanifu na kuunda ndege hiyo ya Aviation Industry Corporation of China (AVIC), kampuni ongozi kwa kuunda ndege nchini humo.
AG600 ni ndege ya kwanza kubwa ya kiraia ya China yenye madhumuni maalum iliyoundwa kulingana na matakwa ya kanuni za kustahiki usafiri wa anga.
Ni aina ya vifaa vikubwa vya angani vilivyoundwa kukidhi mahitaji ya dharura ya mfumo wa kitaifa wa uokoaji wa dharura na mfumo wa kitaifa wa kuzuia na kudhibiti majanga ya asili, kulinda usalama wa maisha na mali za watu.
AG600 ndiyo ndege kubwa zaidi ya kiraia duniani inayoweza kutua kwenye maji katika kipengele cha uzito wa kupaa. Kuundwa kwake kwa mafanikio pia kunajaza pengo la China katika sekta ya ndege kubwa zinazoweza kutua kwenye maji ya China, kwa mujibu wa AVIC.
Umbo lake ni kubwa kidogo kuliko lile la ndege za kawaida za njia moja ya kutenganisha siti za pande mbili zilizo sokoni kwa sasa. Ina urefu wa mita 38.9, kimo cha mita 11.7, na mabawa yenye urefu wa mita 38.8, kwa mujibu wa data kutoka kwa kampuni muundaji.
AG600 ina uzito wa juu wa kupaa angani wa tani 60, na upeo wa juu wa kuruka wa kilomita 4,500. Haswa, inaweza kubeba tani 12 za maji kwa majukumu ya zima moto.
"Kupata cheti chake kilichotolewa na CAAC kunaonyesha kuwa China inaweza kuunda kizazi kipya zaidi duniani cha ndege kubwa za kiraia zinazoweza kutua kwenye maji," mbunifu mkuu wa ndege za AG600 Huang Lingcai ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano maalum.
Eneo kubwa la China lina mandhari tofauti na magumu, ambayo yanahitaji ndege kubwa yenye uwezo wa kuzima moto na majukumu mengine ya uokoaji wa dharura kote nchini.
"AG600 ni ndege inayoweza kuogelea na meli inayoweza kuruka," amesema Huang.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma