Njia ya treni ya mizigo yaunganisha Mji wa Chongqing, China na Asia ya Kati (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 21, 2025
Njia ya treni ya mizigo yaunganisha Mji wa Chongqing, China na Asia ya Kati
Picha iliyopigwa Aprili 20, 2025 ikionyesha treni ya mizigo ya China-Asia ya Kati ikiondoka kutoka Stesheni ya Reli ya Tuanjiecun mjini Chongqing, kusini-magharibi mwa China. (Xinhua/Tang Yi)

CHONGQING - Treni ya mizigo iliyopakiwa chips za polyester zilizotengenezwa katika Mji wa Chongqing, kusini-magharibi mwa China imeondoka kutoka mji huo jana Jumapili asubuhi kuelekea Uzbekistan, ikionesha uzinduzi wa njia mpya ya treni ya mizigo ya usafiri wa kila baada ya muda uliowekwa kutoka Chongqing hadi nchi za Asia ya Kati.

Treni hiyo inatarajiwa kuwasili katika mji mkuu wa Uzbekistan ulio umbali wa kilomita karibia 4,700 katika muda wa siku 12. Itatoka nje ya mipaka ya China kupitia Bandari ya Horgos mjini Xinjiang na kupitia Kazakhstan.

Kampuni ya Kundi la Reli la China huko Chengdu imesema, kila mwezi treni mbili za mizigo zikianza usafiri kutoka Chongqing hadi Asia ya Kati.

Xu Meiqiong, mhandisi wa kampuni hiyo ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwamba huduma hizo za hali ya kawaida zinaweza kuhakikisha kupita forodha kwa haraka, kusafirisha mizigo kwa wakati na kupunguza gharama, ili kuhakikisha usafirishaji wa kuvuka mipaka wenye ubora zaidi.

Imeeleza kuwa njia hiyo ya usafiri wa treni inaweza kupunguza kwa asilimia 30 ya muda wa usafirishaji kati ya Chongqing na Asia ya Kati.

Mizigo iliyopakiwa kwenye treni hiyo ya mizigo jana Jumapili imetoka kwa Kampuni ya Teknolojia za Nyenzo Mpya ya Chongqing Wankai. Lin Zheng, meneja wa kampuni hiyo anayehusika na uchukuzi na usambazaji bidhaa amesema kuwa kuzinduliwa kwa njia hiyo mpya itakuwa nzuri kwao kupanua soko lao katika Asia ya Kati.

Katika miaka ya hivi karibuni, mji huo wa Chongqing umekuwa ukijitahidi kujiinua kuwa kituo jumuishi cha ndani ya bara, huku idadi ya treni za mizigo za China-Ulaya na zile zinazoelekea nchi za Asia ya Kati zinapoongezwa, pia mizigo inayosafirishwa inaongezwa.

Hadi kufikia Februari, zimetumwa treni zaidi ya 18,000 zinazoendeshwa kwenye njia zaidi ya 50 zinazounganisha mji huo na nchi za Ulaya na Asia ya Kati, zikiwasili katika miji na maeneo zaidi ya 100 kote Asia na Ulaya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha