Rais Xi Jinping atilia maanani uhifadhi wa mali ya urithi wa utamaduni na mazingira ya asili ya Fujian

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 20, 2025
Rais Xi Jinping atilia maanani uhifadhi wa mali ya urithi wa utamaduni na mazingira ya asili ya Fujian

‌Mabaki ya kale na mali ya urithi wa utamaduni vimebeba jene na mshipa wa damu za Taifa la China, ni rasilimali bora za ustaarabu wa China ambazo haziwezi kuzaliwa tena na hazina mbadala wake." Mkoa wa Fujian una historia ndefu ya utamaduni na mali nyingi za urithi wa utamaduni usioshikika. Miradi 10 ya Fujian iliwekwa kwenye Orodha ya Mali ya Urithi wa Utamaduni Usioshikika Duniani na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, Mkoa wa Fujian ndio mkoa pekee nchini China uliofanikiwa kupata nafasi nzuri katika miradi mitatu ya uhifadhi wa mali ya urithi wa utamaduni usioshikika.

Rais Xi Jinping siku zote anatilia maanani sana kuhifadhi na kurithisha mali za urithi wa utamaduni usioshikika, akisisitiza kuimarisha uhifadhi wa mali za urithi wa utamaduni usioshikika ili kukidhi vizuri zaidi mahitaji ya utamaduni wa kiroho ya watu yanayoongezeka siku hadi siku, na kuongeza hali ya kujiamini na kujiimarishwa kwa utamaduni wetu.

Tunapaswa kuhimiza utamaduni bora wa jadi wa China kubadilishwa upya na kuendelea kwa ubunifu, na kuimarisha nguvu ya mshikamano wa Taifa la China, kuongeza ushawishi wa utamaduni wa China, kuongeza zaidi mawasiliano na kufundishana kati ya ustaarabu mbalimbali, kusimulia ipasavyo hadithi za utamaduni bora wa jadi wa China, na kusukuma utamaduni wa China uelekee duniani."

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha