Shule za Ghana zaadhimisha Siku ya Lugha ya Kichina ya UN

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 18, 2025
Shule za Ghana zaadhimisha Siku ya Lugha ya Kichina ya UN
Wanafunzi wakijifunza ufundi wa mikono kwenye maadhimisho ya Siku ya Lugha ya Kichina katika Mkoa wa Kati, Ghana, Aprili 16, 2025. (Xinhua/Seth)

ACCRA - Baadhi ya shule katika Mkoa wa Kati wa Ghana na Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Cape Coast (CIUCC) Jumatano waliwasilisha maonyesho ya kuvutia kuadhimisha Siku ya Lugha ya Kichina ya Umoja wa Mataifa, inayoadhimishwa kila mwaka Aprili 20.

Wanafunzi wa lugha ya Kichina katika mkoa huo wamecheza ngoma za simba, kuonyesha sanaa ya Kung Fu na kuimba nyimbo za Kichina kwenye hafla hiyo, wakishangiliwa na watazamaji.

Emmanuel Essuman, mkurugenzi wa mkoa huo wa kati wa Idara ya Elimu ya Ghana, ameipongeza CIUCC kwa ushirikiano wake na kurugenzi hiyo ya elimu ya mkoa ili kuhimiza masomo ya lugha nyingi miongoni mwa wanafunzi katika mkoa huo.

"Kama waelimishaji, tumeitwa kuwa wenye kunyumbulika, kubadilika kuendana na hali, na kuwa na fikra za kutazama mbele katika dunia inayozidi kuwa kuunganishwa. Uwezo wa kutumia lugha na tamaduni mbalimbali si tu faida, bali pia ni jambo la lazima," amesema Essuman.

Amehimiza wanafunzi hao kuendeleza kupenda lugha nyingi kutokana na fursa zinazoweza kujitokeza kutokana na hali hiyo hapo baadaye.

"Kukumbatia lugha hufungua milango kwa uzoefu mpya, utamaduni mpya, na miunganisho mipya ambayo inaweza kuboresha maisha yako," amesema mkurugenzi huyo wa mkoa.

Katika hotuba yake, Balozi wa China nchini Ghana Tong Defa amesisitiza lugha ya Kichina kama daraja la mawasiliano na ufunguo wa dhahabu wa kuzidisha maelewano na kukuza ushirikiano.

"Katika miaka ya hivi karibuni, elimu ya lugha ya Kichina nchini Ghana imestawi. Kama jukwaa muhimu la mabadilishano ya kitamaduni kati ya China na Ghana, Taasisi za Confucius zimejenga wanafunzi wengi bora," Tong amesema.

"China na Ghana zimekuwa zikifurahia urafiki wa jadi kwa muda mrefu, na sasa wamekuwa wenzi wa kimkakati. Uhusiano huo wa karibu na wa kirafiki umeleta manufaa makubwa kwa nchi zetu mbili na watu wake. Haungeweza kufikiwa bila jitihada za ndugu za Ghana ambao wamekuwa wajuvi wa lugha ya Kichina," balozi huyo ameongeza.

Wawakilishi kutoka jamii ya Wachina nchini Ghana na viongozi wa zamani na waelimishaji wa Ghana pia walishiriki kwenye hafla hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha