Jimbo la California, Marekani lashtaki serikali ya Trump kutoza ushuru "usio wa kisheria"

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 18, 2025
Jimbo la California, Marekani lashtaki serikali ya Trump kutoza ushuru
Waandamanaji wakiandamana dhidi ya sera tata zilizoanzishwa na utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump katika Grand Park, katikati mwa Los Angeles, California, Marekani, Aprili 5, 2025. (Picha na Qiu Chen/Xinhua)

LOS ANGELES - Jimbo la California la Marekani siku ya Jumatano limefungua kesi ya kisheria ya serikali kuu kuzuia ushuru uliotozwa na utawala wa Trump, likidai kuwa sera hiyo inaumiza familia, biashara ndogo na uchumi wa jimbo hilo.

"Hakuna jimbo lolote ambalo litapoteza zaidi kuliko jimbo la California," Gavana wa California Gavin Newsom amesema akiwa kwenye shamba la njugu za mlozi katika Bonde la Kati siku ya Jumatano, akiongeza kuwa hali ya kutokuwa na uhakika juu ya kiasi gani jimbo hilo linaweza kuathirika kutokana na ushuru huo "iko dhahiri na kubwa," kwani lozi, pistachios na bidhaa za maziwa ni bidhaa zinazouzwa nchi za nje kwa wingi za jimbo hilo.

"Ushuru usio wa kisheria wa Rais Trump unaleta vurugu kwa familia, biashara za California na uchumi wetu -- ukiongeza bei na kutishia ajira," Newsom amesema katika taarifa. "Tunasimama kutetea familia za Marekani ambazo haziwezi kuvumilia kuruhusu hali hiyo iendelee."

Kesi hiyo, iliyofunguliwa kwenye Mahakama ya Wilaya ya Marekani kwa Wilaya ya Kaskazini ya California, imelenga Trump kutumia Sheria Dharura ya kiuchumi ya Kimataifa, sheria hiyo ya mwaka 1977 iliyokusudiwa kwa misukosuko ya nje, na si kwa ajili ya kuweka ushuru, Newsom amesema, akifafanua kuwa Bunge la Marekani pekee ndilo lenye mamlaka ya kuweka ushuru.

"Donald Trump hana mamlaka ya kutoza ushuru huu wenye uharibifu mkubwa na wenye vurugu. Marekani iko kwenye mazingira ya kupoteza sana," gavana huyo amesema katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii X.

Jimbo hilo ni muuzaji nje mkubwa zaidi wa bidhaa za kilimo na mwagizaji mkubwa zaidi wa bidhaa kutoka nje nchini Marekani.

"Wanacalifornia wanajiandaa kwa ajili ya athari za maamuzi ya rais -- yakiathiri kila mtu kutoka wakulima katika Bonde la Kati hadi biashara ndogo mjini Sacramento, vilevile familia zenye wasiwasi kwenye meza zao za chakula cha jioni," Mwanasheria Mkuu wa California Rob Bonta amesema Jumatano.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha