

Lugha Nyingine
Upanuzi wa uwanja wa ndege mkoani Xinjiang, China waongeza ufunguaji mlango wa ngazi ya juu
URUMQI – Jengo jipya la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Urumqi Tianshan, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini-magharibi mwa China limeanza kufanya kazi rasmi jana Alhamisi, ikionyesha hatua kubwa katika kupanua uwezo wa anga wa mkoa huo.
Jengo hilo ni sehemu muhimu ya mradi wa upanuzi wa uwanja huo ulioanza mwaka 2019. Baada ya upanuzi huo, uwezo wa kupitisha abiria na mizigo wa uwanja huo, ambao zamani ulijulikana kwa jina la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Urumqi Diwopu, umeongezeka zaidi ya mara tatu kwa mwaka, na utakuwa kituo cha anga cha China kufungua mlango kuelekea sehemu za magharibi, Kundi la Kampuni za Uwanja wa Ndege wa Xinjiang limeeleza.
Kufuatia kukamilika kwa mradi huo wa upanuzi, uwanja huo wa ndege sasa una njia tatu za kuruka na kutua ndege, na unaweza kuhudumia abiria hadi milioni 48 na tani 550,000 za mizigo kwa mwaka. Sasa una uwezo wa kupaa na kutua ndege karibu 367,000.
"Baada ya jengo hilo jipya kuzinduliwa, uwanja wa ndege wa Urumqi utatoa huduma za kiwango cha juu zaidi, zenye ufanisi zaidi za usafiri wa anga na kutoa mchango mkubwa zaidi katika kupanua ufunguaji mlango wa kiwango cha juu na kuhimiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya kikanda," Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya China (CAAC) imesema.
Ukiwa ulianzishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1939, uwanja huo wa ndege umepitia upanuzi mkubwa mara nne, huku uboreshaji wake wa hivi karibuni ukiwa umekamilika mwaka huu.
Kwa mujibu wa CAAC, serikali kuu ya China imetenga yuan zaidi ya bilioni 12 (sawa na dola za kimarekani takriban bilioni 1.66) kutoka kwa mfuko wa maendeleo ya usafiri wa anga ili kuunga mkono maendeleo ya muda mrefu ya uwanja huo wa ndege. Aidha, yuan bilioni 3 kutoka kwenye bajeti kuu ya China pia zimewekezwa kuboresha uwanja huo wa ndege.
Kutokana na kupanuliwa kwa uwezo na kuimarika kwa mawasiliano na muunganisho, uwanja huo wa ndege unabadilika kutoka lango la kikanda hadi kuwa daraja linalounganisha China na Asia ya kati na magharibi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Sosholojia katika Akademia ya Sayansi ya Jamii ya Xinjiang, Yang Fuqiang, amesema upanuzi huo si tu uboreshaji wa miundombinu rahisi, pia utaleta fursa zaidi na uwezekano wa maendeleo ya kiuchumi ya mkoa huo wa Xinjiang, na ushirikiano wa kimataifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma