

Lugha Nyingine
China yajiandaa kurusha chombo cha Shenzhou-20 cha kuwabeba wanaanga kwenda anga ya juu
(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 17, 2025
JIUQUAN – Chombo cha Shenzhou-20 cha kuwabeba wanaanga na roketi ya kubeba ya Long March-2F kwa pamoja vimehamishiwa kwenye eneo la kurusha vyombo kwenda anga ya juu, Shirika la Anga ya Juu la China (CMSA) limesema jana Jumatano.
Shirika la CMSA limesema, majengo na vifaa vyote viko katika hali nzuri kwenye eneo hilo la kurushia vyombo kwenda anga ya juu, wakati huohuo ukaguzi wa kazi za kabla ya urushaji na majaribio ya pamoja yatafanywa kama ilivyopangwa.
“Chombo hicho kitarushwa kwa mpango uliowekwa” Shirika la CMSA limesema.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma