Xi Jinping na simulizi ya chai ya Fujian (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 17, 2025
Xi Jinping na simulizi ya chai ya Fujian

Mkoa wa Fujian ukiwa eneo muhimu la ustawi wa chai katika nchi ya China, utamaduni wa chai wa Fujian una historia ndefu. Mapema alipokuwa akifanya kazi mkoani Fujian, Xi Jinping aliichukulia shughuli za chai za eneo hilo kuwa moja ya shughuli saba muhimu zenye nguvu bora zinazopaswa kuendelezwa na kuhimizwa kwa uangalifu, na alifanya utafiti katika maeneo yote muhimu ya kilimo cha chai.

Tokea Mkutano Mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China, Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC amekuwa akitembelea mashamba ya chai mara nyingi wakati wa ziara za ukaguzi katika serikali za mitaa na kuelekeza maendeleo mazuri ya shughuli za chai.

Wakati wa ziara yake ya ukaguzi mkoani Fujian, Katibu Mkuu Xi alisisitiza kwamba "Lazima kufanya mpango wa jumla wa kufanya kazi nzuri katika utamaduni wa chai, shughuli za chai, na teknolojia ya chai.""Huko nyuma, shughuli za chai zilikuwa nguzo ya kupunguza umaskini hapa, na katika siku zijazo zitakuwa nguzo ya kustawisha vijiji."

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha