China yazindua mradi wa kwanza wa mafunzo ya teknolojia ya Juncao nchini Zimbabwe (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 16, 2025
China yazindua mradi wa kwanza wa mafunzo ya teknolojia ya Juncao nchini Zimbabwe
Mwanamke akiangalia nyasi za Juncao kwenye mafunzo ya teknolojia ya Juncao uliotolewa kwa msaada wa China katika Jimbo la Mashonaland Magharibi, Zimbabwe, Aprili 14, 2025. (Xinhua/Tafara Mugwara)

HARARE - Mradi wa kwanza wa mafunzo ya teknolojia ya Juncao uliotolewa kwa msaada wa China umezinduliwa katika Jimbo la Mashonaland Magharibi nchini Zimbabwe jana Jumatatu ili kusaidia kuhimiza maendeleo ya kilimo katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika ambapo washiriki zaidi ya 50 wakiwemo wakulima, wanafunzi na wasomi wameshiriki kwenye mafunzo hayo ya siku tatu, ambayo imehusisha vyote vipindi vya kinadharia na kuonyesha kivitendo kwa wataalamu wa kiufundi wa China.

Juncao ni nyasi chotara na rasilimali ya kilimo yenye matumizi mengi iliyovumbuliwa na kuendelezwa nchini China na kuenezwa duniani kote.

Rao Huohuo, kiongozi wa timu ya teknolojia ya Juncao ya msaada wa China nchini Zimbabwe, amesema mradi huo wa miaka mitatu utawezesha wakulima wenyeji kufahamu kikamilifu teknolojia ya Juncao katika nyanja nyingi, zikiwemo upandaji wa Juncao na matumizi katika kukuza uyoga na kulisha mifugo.

Mandiudza Masvongo, mkulima mdogo na mshiriki katika programu hiyo ya mafunzo, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kuwa ana mpango wa kulima Juncao kwa matumizi ya chakula cha mifugo.

"Maeneo yetu ya malisho yanakuwa machache kutokana na mchakato wa utandawazi wa miji na mabadiliko ya Tabianchi. Hivyo ni faida kulima Juncao kwa sababu katika shamba langu, ninaweza kutumia kikamilifu hekta moja tu kulima nyasi ili mifugo yangu ipate malisho ya kutosha," amesema.

Masvongo pia ameelezea matarajio ya kutumia teknolojia hiyo ya Juncao kwa kilimo endelevu cha uyoga wa chakula kama njia ya kuongeza kipato cha familia yake.

Mshiriki mwingine, Yeukai Chimbi, mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Zimbabwe, amesema amefahamu kwamba teknolojia ya Juncao inaweza kutumika kupunguza baadhi ya changamoto zinazokabili wakulima nchini humo.

"Kwa mfano, nyasi za Juncao husaidia katika kurejesha ardhi iliyoharibiwa, hivyo labda hapa Zimbabwe, tunaweza kuikuza katika maeneo ambayo kuna hali ya kuenea kwa jangwa," amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha