

Lugha Nyingine
Mlima Heidu katika Mkoa wa Qinghai, China: “Mwezi Duniani” (4)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 16, 2025
Mlima Heidu uliopo Mji mdogo wa Lenghu, Mji wa Mangya, Mkoa wa Qinghai, China, huonekana kama mchoro wa wino katika mazingira ya asili, ukitanda kwenye Jangwa kubwa la Gobi.
Kuundwa kwa Mlima Heitu ni matokeo ya mamilioni ya miaka ya mabadiliko ya kijiolojia na mmomonyoko uliosababishwa na upepo. Mawe yenye kiasi kikubwa cha madini kama vile chuma na Manganese, hatua kwa hatua huonesha rangi nzito nyeusi chini ya mmomonyoko wa muda mrefu uliosababishwa na upepo, ikiunda utofauti mkubwa na mazingira ya karibu. Muundo wake wa kipekee wa ardhi ya Yardang yenye rangi nyeusi, husifiwa na watu kama “Mwezi Duniani”.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma