

Lugha Nyingine
Jangwa la Taklimakan la Xinjiang, China lazungukwa na ukanda wa kijani kwa sababu ya juhudi za kudhibiti mchanga (4)
![]() |
Picha iliyopigwa Aprili 12, 2025 ikionesha mbuga katika Wilaya ya Beicheng, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, China. (Xinhua/Ding Lei) |
Jangwa la Taklimakan lililopo Mkoa wa Xinjiang, China linaenea kwenye eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 337,600, na mzunguko wake unafikia kilomita 3,046, ikilifanya kuwa jangwa kubwa zaidi nchini China na jangwa la pili kwa ukubwa duniani lenye kusogea kutoka sehemu yake.
Shukrani kwa juhudi za miongo kadhaa za kuzuia na kudhibiti mchanga, Jangwa hilo la Taklimakan lilizungushwa kikamilifu na ukanda wa kijani unaozuia mchanga Novemba 28, 2024.
Katika mwaka 2025, mkoa huo wa Xinjiang unalenga kupanda msitu kwenye eneo lenye ukubwa wa hekta 796,000, zikiwemo hekta 562,666 kwa ajili ya udhibiti wa mstari wa mbele katika Jangwa la Taklimakan. Upandaji huo wa msitu ni sehemu ya Mradi wa Misitu ya Ukanda wa Ulinzi wa Ikolojia wa Maeneo Matatu ya Kaskazini mwa China, ambao ni mradi mkubwa zaidi wa upandaji msitu duniani unaoshughulikia hali ya kuenea kwa jangwa Kaskazini Magharibi, Kaskazini na Kaskazini Mashariki mwa China.
Wakati huohuo, mkoa huo wa Xinjiang utapanua zaidi ukanda huo wa kijani wa kuzuia mchanga na kuongeza juhudi za kufunga mchanga ili kufikia udhibiti endelevu wa mchanga na wakati huohuo ukiboresha maisha ya wakazi wenyeji.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma