Mji wa Nyingchi, Mkoani Xizang wahimiza Utalii kwa safari za kutazama maua (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 14, 2025
Mji wa Nyingchi, Mkoani Xizang wahimiza Utalii kwa safari za kutazama maua
Wanakijiji wakiwa tayari kuonesha shughuli za mila na desturi kwa watalii huko Nyingchi, mkaoni Xizang, China Aprili 3, 2025. (Xinhua/Tenzin Nyida)

Katika miaka ya hivi karibuni, Mji wa Nyingchi umejumuisha utazamaji maua katika maendeleo ya utalii, ukijitahidi kubadilisha mandhari yake nzuri kuwa rasilimali ya kiuchumi.

Takwimu zinaonesha kuwa kuanzia tarehe 4 hadi 6 Aprili, 2025, mji huo ulipokea watalii 208,600, idadi ambayo imeongezeka kwa asilimia 20.58 kuliko mwaka jana kipindi kama hicho. Mapato yake ya utalii yamefikia Yuan milioni 150 (sawa na dola za Marekani milioni 20.5 hivi), yakiongezeka kwa asilimia 37.62 kuliko mwaka jana kipindi kama hicho.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha