Wilaya ya Beilun ya Mji wa Ningbo, China yatekeleza mipango ya maendeleo kwa minyororo ya kiviwanda

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 11, 2025
Wilaya ya Beilun ya Mji wa Ningbo, China yatekeleza mipango ya maendeleo kwa minyororo ya kiviwanda
Kreni ikipakia makontena kwenye kampuni ya usambazaji bidhaa katika Wilaya ya Beilun ya Mji wa Ningbo, Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China, Aprili 10, 2025. (Xinhua/Zheng Huansong)

Katika miaka ya hivi karibuni, Wilaya ya Beilun ya Mji wa Ningbo, Mkoa wa Zhejiang imekuwa ikitekeleza mipango yake ya maendeleo ya minyororo muhimu ya kiviwanda, ikiboresha kiwango cha mageuzi ya kidijitali miongoni mwa kampuni za viwanda katika mkoa huo, ikilenga kuendeleza idadi kadhaa ya makundi ya kiviwanda na kampuni ongozi za viwanda zenye faida.

Mwaka 2024, thamani ya jumla ya pato la uzalishaji kwa kampuni za viwanda za ukubwa zaidi ya uliowekwa katika Wilaya hiyo ya Beilun ilikuwa yuan bilioni 585.727 (sawa na dola za Kimarekani bilioni 80.1), ikiwa ni ongezeko la asilimia 9.6 kuliko mwaka jana wakati kama huo. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha