Nchi Wanachama wa SCO zatia saini makubaliano ya ushirikiano wa kiviwanda yenye thamani ya Yuan bilioni 4.8 mjini Tianjin, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 11, 2025
Nchi Wanachama wa SCO zatia saini makubaliano ya ushirikiano wa kiviwanda yenye thamani ya Yuan bilioni 4.8 mjini Tianjin, China
Wageni wakishiriki kwenye hafla ya kutia saini kwenye Mkutano wa China na SCO wa Ushirikiano wa Viwanda vya Maendeleo Endelevu uliofanyika Tianjin, kaskazini mwa China, Aprili 10, 2025. (Xinhua/Zhao Zishuo)

TIANJIN - Mkutano wa China na SCO wa Ushirikiano wa Viwanda vya Maendeleo Endelevu uliofanyika katika Mji wa Tianjin kaskazini mwa China jana Alhamisi, ambapo nchi wanachama wanane wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) zimesaini makubaliano ya ushirikiano yenye thamani ya jumla ya karibu yuan bilioni 4.8 (dola za Kimarekani karibu milioni 665.82).

Pande mbili zimesaini makubaliano ya miradi 18, na kuweka mkazo katika maeneo muhimu kama vile nishati mpya, raslimali mpya, miundombinu, uchimbaji madini na kemikali za petroli.

Washiriki wameeleza kuwa nchi wanachama wa SCO zinaweza kusaidiana katika sekta zenye nguvu bora ya maendeleo endelevu, vilevile kuna uwezekano mkubwa wa ushirikiano wa kiviwanda, hasa katika maeneo ya ujenzi wa miundombinu, uhuishaji wa maliasili za nishati na madini, uchumi wa kidigitali, na viwanda vya teknolojia za kisasa.

Sohail Khan, naibu katibu mkuu wa SCO amesema kuwa mkutano huo ni fursa ya kutimiza matarajio na kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo endelevu ya kikanda.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha