China yazindua mashine kubwa ya kuchimba handaki kwa mradi katika Mto Yangtze (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 11, 2025
China yazindua mashine kubwa ya kuchimba handaki kwa mradi katika Mto Yangtze
Fundi wakifanya kazi kwenye chumba cha uendeshaji cha mashine kubwa ya kuchimba handaki ya "Jianghai" inayojiendelezwa na kutengenezwa na China yenyewe kwa ajili ya ujenzi wa Handaki la Haitai la Yangtze, mjini Haimen, Mkoani Jiangsu, mashariki mwa China, Aprili 9, 2025. (Xinhua/Ji Chunpeng)

NANJING - China Jumatano imeanza kutumia mashine kubwa ya kuchimba handaki ambayo imeendelezwa na kutengenezwa na China yenyewe(TBM) kwa ajili ya ujenzi wa handaki refu zaidi duniani la TBM la barabara kuu ya chini ya maji ambapo mashine hiyo mpya, iliyopewa jina la "Jianghai," ina kipenyo cha juu cha kuchimba cha mita 16.6, urefu wa mita takriban 145 na uzito wa tani 5,000.

Mashine hiyo inatumika katika ujenzi wa Handaki la Haitai la Mto Yangtze katika Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China. Handaki hilo ni mradi muhimu wa kutengeneza barabara kuu kiunganishi ya kuvuka mto chini ya mto huo mrefu zaidi wa China, ikiunganisha Haimen katika mji wa Nantong na Taicang katika mji wa Suzhou.

Likiwa na urefu wa kilomita takriban 39.07, handaki hilo linajumuisha sehemu ya chini ya maji yenye urefu wa kilomita 11.185, huku mita 9,315 zikichimbwa kwa kutumia TBM. Limesanifiwa kuwa na njia sita za kupitisha magari, barabara kuu ya uelekeo wa pande mbili ikiwa na kikomo cha magari kuendeshwa kwa kasi ya kilomita 100 kwa saa.

Likivuka kupita miundo migumu ya kijiolojia chini ya mto, zikiwemo tabaka za matope na mchanga, handaki hilo litafikia kina cha juu cha mita 75, ikiliweka chini ya shinikizo kubwa ambayo ni sawa na tani 75 kwa kila mita ya mraba, kwa mujibu wa You Shaoqiang, mhandisi mkuu wa mradi wa handaki wa Kampuni ya 14 ya Shirika la Reli la China.

"Hali hizi ngumu hufanya mchakato wa ujenzi kuwa na changamoto kubwa," amesema.

Ili kukabiliana na hali ngumu kama hiyo ya ujenzi, mashine hiyo ya "Jianghai" imefungwa teknolojia vumbuzi, kikiwemo kifaa cha msawazisho wa shinikizo cha kuchimbua kwa mbele na mfumo wa kisasa wa ufuatiliaji unaowezesha ufuatiliaji kwa wakati halisi wa ufungaji visu vya kuchimbua kwa mbele na kurahisisha kazi ya kutengeneza na kubadilisha visu vya kuchubuandani ya chumba cha kufanyia kazi chini ya maji. Pia ina sindano mbili za kutopesha udongo ili kuboresha ufanisi," amesema meneja wa mradi huo wa TBM Meng Defeng.

Handaki hilo linatarajiwa kukamilika mwaka 2028. Baada ya kukamilika, litatumika kama kiungo muhimu kuwezesha usafiri katika Delta ya Mto Yangtze.

"Mradi huu utatoa mchango mkubwa katika kuendeleza ushirikiano kati ya mikoa ndani ya Delta ya Mto Yangtze na kuingiza kasi kubwa katika maendeleo bora ya hali ya juu ya kundi la miji la kiwango cha kimataifa la Delta la Mto Yangtze," You amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha