Wanafunzi wa Tanzania wakumbatia lugha ya Kichina kutokana na mahitaji yanayoletwa na ustawi wa utalii (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 10, 2025
Wanafunzi wa Tanzania wakumbatia lugha ya Kichina kutokana na mahitaji yanayoletwa na ustawi wa utalii
Wanafunzi wa Tanzania wakishiriki kwenye somo la lugha ya Kichina katika Chuo cha Taifa cha Utalii cha Tanzania jijini Dar es Salaam, Tanzania, tarehe 8 Aprili 2025. (Xinhua/Emmanuel Herman)

DAR ES SALAAM - Akiwa ameketi kwenye darasa la kawaida, mwanafunzi wa utalii nchini Tanzania Noel Ivon Isack alikuwa akifuatilia kwa makini maandishi ya lugha ya Kichina kwenye daftari lake. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 19 anatamani kutumia kikamilifu ujuzi wake mpya wa lugha hiyo ili kujenga taaluma ya kuongoza watalii kupitia hifadhi maarufu za wanyamapori na fukwe zenye mandhari nzuri za Tanzania.

“Ninataka kufanya watalii wa China wahisi wako nyumbani,” anasema Isack, mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo cha Taifa cha Utalii cha Tanzania (NCT) jijini Dar es Salaam. "Wengi wao huzungumza Kichina pekee, hivyo kama tukitaka wafurahie Tanzania, ni lazima tuongee lugha yao."

Kutokana na kuongezeka kwa wimbi la watalii kutoka China, chuo hicho cha utalii cha serikali ya Tanzania kimezindua kozi za lugha ya Kichina kwa kushirikiana na Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ili kuwaandaa watu wenye ujuzi wa sekta hiyo katika siku za baadaye. Kati ya wanafunzi 531 waliodahiliwa kwa sasa, 215 wamechagua kusoma Kichina.

"Hii imebadilisha hali ya sekta hiyo," amesema Farida Sebastian Masalu, meneja wa chuo hicho. "Tunataka kuwapa wanafunzi wetu makali ya ushindani wakati Tanzania ikiimarisha uhusiano na China."

Tangu mwaka 2023, Tanzania imekuwa ikiongeza juhudi za kuvutia watalii kutoka China. Hatua moja kubwa ni kuzinduliwa filamu ya utangazaji utalii ya “Amazing Tanzania” mjini Beijing mwezi Mei 2024, iliyowashirikisha Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi, na mwigizaji wa China Jin Dong.

“Mipango hiyo inakuza utalii wa Tanzania na kuzidisha urafiki kati ya nchi zetu,” Masalu amesema.

Tanzania tayari inashuhudia matokeo. Kwa mujibu wa Ephraim Mafuru, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), watalii waliowasili Tanzania kutoka China waliongezeka kutoka 44,000 hadi 62,000 katika kipindi cha miezi tisa iliyopita.

"Lengo letu ni kuvutia angalau asilimia 1 ya wasafiri wa kimataifa wa China," amesema Mafuru. "Hiyo ni watalii milioni 1.3, na ndiyo tunaanza tu."

Ili kuunga mkono azma hiyo, TTB imekuwa ikishirikiana na taasisi za ndani kama vile NCT kutoa mafunzo ya lugha ya Kichina kwa waongoza watalii na wafanyakazi katika mnyororo mpana wa thamani wa utalii.

"Kizuizi cha lugha kinaendelea kuwa moja ya changamoto zetu kubwa," Mafuru amesema. "Lakini tunakifanyia kazi. Wageni wa China watahisi vizuri zaidi kukaribishwa kwa lugha yao."

Asha Fum Khamis, mwalimu wa lugha ya Kichina aliyetumwa na Taasisi ya Confucius kufundisha katika NCT, ameunga mkono maoni hayo. "Sifundishi lugha tu," amesema. Ninatayarisha wanafunzi hawa kwa fursa halisi, zikiwemo za kazi, ushirikiano, na madaraja ya utamaduni."

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha