Maonyesho ya 13 ya Teknolojia ya Upashanaji Habari ya China yaanza mjini Shenzhen

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 10, 2025
Maonyesho ya 13 ya Teknolojia ya Upashanaji Habari ya China yaanza mjini Shenzhen
Watu wakitembelea kwenye Maonyesho ya 13 ya Teknolojia ya Upashanaji Habari ya China (CITE 2025) mjini Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, Aprili 9, 2025. (Xinhua/Liang Xu)

Maonyesho ya 13 ya Teknolojia ya Upashanaji Habari ya China (CITE 2025) yameanza kwenye Kituo cha Mikutano na Maonyesho cha Shenzhen (Futian) jana Jumatano mjini Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China.

Yakiwa na kaulimbiu ya "Teknolojia Inaongoza, Uvumbuzi Kukusanyika Shenzhen", maonyesho hayo yanaangazia zaidi maeneo muhimu ya teknolojia mpya za kisasa kama vile vifaa mahiri vya kuchakata na kupeleka habari, maonyesho ya vifaa vya macho, akili bandia, uhifadhi data kubwa, vifaa vya msingi, na uchumi wa anga ya chini, yakivutia kampuni zaidi ya elfu moja kushiriki kwenye maonesho. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha