Ushirikiano wa kiteknolojia wa China-Afrika wasifiwa kama mpango wa kuboresha mfumo wa chakula wa Afrika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 09, 2025
Ushirikiano wa kiteknolojia wa China-Afrika wasifiwa kama mpango wa kuboresha mfumo wa chakula wa Afrika
Watu wakishiriki kwenye shughuli katika wakati wa Wiki ya Sayansi ya Kikundi cha Utafiti na Mashauriano juu ya Kilimo cha Kimataifa inayoendelea jijini Nairobi, Kenya, Aprili 8, 2025. (Xinhua/Han Xu)

NAIROBI - Kuanzisha jukwaa la kuhamisha teknolojia na uvumbuzi kwa kupitia ushirikiano kati ya China na Afrika ni muhimu sana kwa ajili ya kuboresha mifumo ya chakula ya Afrika katika hali ya kuwepo kwa matatizo ya tabianchi, wadudu waharibifu, magonjwa na kupungua kwa rutuba ya udongo, wanasayansi na viongozi wahusika wamesema jana Jumanne.

Wakizungumza kwenye shughuli katika wakati wa Wiki ya Sayansi ya Kikundi cha Utafiti na Mashauriano juu ya Kilimo cha Kimataifa inayoendelea jijini Nairobi, Kenya, washiriki wamesema kwamba kutumia teknolojia ya kurutubisha mbegu za mimea, kudhibiti wadudu na umwagiliaji kutawezesha bara hilo kushughulikia janga la njaa linaloendelea.

Shughuli hiyo yenye kaulimbiu ya "Kujenga Madaraja," iliandaliwa na Jumuiya ya Utafiti na Mashauriano ya Kilimo cha Kimataifa CGIAR na washirika wake, ikiwa ni pamoja na kampuni ya China ya jenomiki ya Kundi la BGI, moja ya mashirika yanayoongoza duniani ya sayansi ya uhai wa maisha na jenomiki, kuchunguza maeneo mapya ya ushirikiano katika kilimo na uhifadhi wa bioanuwai.

Mkurugenzi Mkuu wa CGIAR Ismahane Elouafi ametoa wito wa kutumia teknolojia ya AI, jenomiki na nanoteknolojia ili kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao na ufugaji wa mifugo barani Afrika katika wakati wa msukosuko wa njaa na utapiamlo uliosababishwa na tabianchi.

Amesisitiza kuwa ili kupunguza gharama ya kuagiza chakula barani humo, ambayo kwa sasa inafikia dola za kimarekani takriban bilioni 100 kila mwaka, uwekezaji katika afya ya udongo, usimamizi wa raslimali za maji na kuandaa mbegu kwa kutumia mimea ya aina za mazao yenye mavuno mengi ni muhimu.

Wang Jian, mwanzilishi mwenza na mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kundi la BGI, amesema, kwa "kutumia teknolojia ya kisasa kupima mpangilio na miundo ya AI, BGI ina uwezo wa kuweka kidijitali mamilioni ya sampuli za vijidudu zilizokusanywa na watafiti duniani kote."

Mkurugenzi wa Utafiti wa BGI Xu Xun amesema kuwa kuimarisha ushirikiano na CGIAR kutakuza uwekaji kidijitali wa viini vya magonjwa, kuongeza kasi ya kuandaa mbegu za mazao, na kuimarisha ustahimilivu wa mfumo wa chakula katika nchi zinazoendelea, hasa barani Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha