

Lugha Nyingine
Mlinzi akua pamoja na panda Sichuan, China (2)
Akiwa mzaliwa wa Mkoa wa Sichuan, unaojulikana kama maskani ya panda, Li amekuza uhusiano maalum na panda tangu utotoni. Akisukumwa na shauku yake ya kuchunguza mazingira ya asili na kufuatilia wanyama pori, alisoma elimu ya uhifadhi wa wanyamapori katika chuo kikuu.
Baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu, Li alianza kufanya kazi katika fani zingine, lakini mwaka 2019, alipojua kuwa kituo hicho cha panda kilikuwa kikiajiri watunzaji, alituma maombi ya kazi ili kurejea ndoto aliyokuwa ameisimamisha.
"Hapo awali, panda wote walionekana kufanana kwangu. Lakini baada ya kuwa mlinzi, nimegundua kuwa wanatofautiana kabisa," Li amesema.
Pia amesema kuwa kutunza panda kunahitaji umakini zaidi kuliko kulea watoto -- kuanzia kusafisha nzio na kuandaa chakula hadi kutazama na kurekodi. Kazi hufanya saa kupita haraka.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma