

Lugha Nyingine
Rais wa Tanzania azindua makao makuu ya mahakama
DAR ES SALAAM - Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania amezindua jengo jipya la makao makuu ya mahakama ya Tanzania katika mji mkuu Dodoma, ambalo limejengwa na Kampuni ya Uhandisi ya Jianchang ya Shirika la Reli la China (CRJE) (Afrika Mashariki), kampuni inayogonza ya ujenzi ya China.
Jengo hilo la makao makuu ya mahakama ya Tanzania ni maskani ya matawi matatu ya juu zaidi ya mahakama ya Tanzania: Mahakama Kuu, Mahakama ya Rufani na Mahakama ya Juu. Jengo hilo alama lenye orofa tisa, linalochukua eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 63,244, lina huduma za akili mnemba, roboti za kuongoza wageni na sehemu maalum ya kupaa na kutua helikopta.
Akizungumza baada ya kuzindua jengo hilo la Mahakama juzi Jumamosi, Rais Samia amesema kuwa makao makuu hayo mapya ya mahakama yanapaswa kutumika kuimarisha usimamizi wa utoaji haki nchini humo.
“Uwekezaji huu mkubwa, sambamba na programu zinazoendelea za mafunzo kwa majaji na maafisa wa mahakama, unaonyesha dhamira ya serikali katika kuimarisha uwezo na ufanisi wa mahakama,” amesema.
Mwenyekiti wa Kampuni ya CRJE (Afrika Mashariki), Jiang Yuntao, amesema tangu kushiriki katika ujenzi wa Reli ya Tanzania na Zambia mwaka 1969, CRJE imeendelea kuwa na dhamira kubwa ya kuleta maendeleo nchini Tanzania.
Jijini Dodoma, kampuni hiyo imeshakabidhi miradi alama ikiwemo Jengo la Bunge la Tanzania, Chuo Kikuu cha Dodoma, ghorofa la PSSSF na Makao Makuu ya Wizara ya Maji.
Jiang amesema kuwa kampuni hiyo itaendelea kuunga mkono ukuaji wa mji mkuu huo na maendeleo ya kijamii na kiuchumi kupitia ujenzi bora na kuwaandaa wenyeji wenye ujuzi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma