

Lugha Nyingine
Kipindi cha Opera za China 2025 chaanza Vienna, Austria
![]() |
Wasanii wakifanya maonesho ya mchezo wa sanaa wa Opera ya Lahaja ya Wu “Hadithi ya Nyoka Mweupe” huko Vienna, mji mkuu wa Austria, Aprili 5, 2025. (Picha na Zhao Dingzhe/Xinhua) |
VIENNA - Kipindi cha maonesho ya michezo ya sanaa ya Opera za China 2025 kimeanza mjini Vienna, juzi Jumamosi usiku kwa mchezo wa sanaa wa Opera ya kijadi ya lahaja ya Wu ya “Hadithi ya Nyoka Mweupe”, ukionesha mwanzo wa mfululizo wa maonyesho ya michezo ya sanaa ya opera za China katika mji mkuu huo wa Austria.
Jumla ya michezo ya sanaa ya Opera nane za China za mitindo ya aina mbalimbali itaonyeshwa mjini Vienna katika kipindi hiki cha mwaka huu, ikiwemo pamoja na Opera ya Kunqu na Opera ya Yue.
Ming Wenjun, Mkuu wa Jumuiya ya Utafiti wa Michezo ya Sanaa ya Opera za China, amefungua rasmi kipindi hiki cha maoensho, akieleza kwamba michezo ya sanaa ya Opera za China za aina mbalimbali inaonyesha thamani ya msingi ya hali ya masikilizano ya aina mbalimbali za utamaduni wa China.
Maonesho ya kufunguliwa kwa kipindi hiki yalifanyika kwenye ukumbi wa matamasha wa Das MuTh wa Vienna, yakionesha vilivyo simulizi ya kimahaba kuhusu nyoka mweupe aliyebadilika kuwa mwanamke Bai Suzhen na mapenzi yake kwa kijana Xu Xian.
Michezo ya sanaa ya Opera za lahaja za Wu ilianzia katika Enzi ya Ming (1368-1644), Opera hizo zinajulikana sana kwa mchanganyo wake wa vipande vya matukio ya kivitendo na maonesho murua ya Opera za kijadi za China zinazovutia watu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma