Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Utawala ya Myanmar atoa shukrani kwa timu za uokoaji za China (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 07, 2025
Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Utawala ya Myanmar atoa shukrani kwa timu za uokoaji za China
Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Utawala ya Myanmar (SAC) Min Aung Hlaing (wa kwanza kulia, mbele) akitembelea kambi ya timu za uokoaji za China, Mandalay, Myanmar, Aprili 6, 2025. (Xinhua/Cai Yang)

MANDALAY, Myanmar - Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Utawala ya Myanmar (SAC) Min Aung Hlaing ametembelea kambi ya timu za uokoaji za China mjini Mandalay jana Jumapili, ili kutoa shukrani zake kwa watu wote wa Timu ya Utafutaji na Uokoaji ya China, Timu ya Kimataifa ya Utafutaji na Uokoaji ya China, na timu ya uokoaji kutoka Hong Kong ya China kwa nguvu zao kubwa za kusaidia kuwaokoa watu nchini Myanmar baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi la 7.9.

“Kuwasili kwa timu za uokoaji za China kutoa uungaji mkono kutoka mbali kumeonyesha urafiki mkubwa wa "Paukphaw" (kidugu) kati ya nchi hizo mbili,” Min Aung Hlaing amesema.

Amesema, timu za uokoaji za China zina uzoefu mkubwa katika shughuli za utafutaji na uokoaji za kuvuka mipaka, na Myanmar inatarajia kuimarisha mawasiliano na China ili kupanua ushirikiano katika kukabiliana na hali ya dharura, juhudi za kuzuia na kupunguza athari za maafa.

Konsuli Mkuu wa China katika mji huo wa Mandalay, Gao Ping na Mkuu wa Eneo la Mandalay U Myo Aung walikuwepo kwenye mkutano huo. Hadi kufikia Aprili 6, timu hizo za uokoaji za China zilikuwa zimeshafanikiwa kuokoa manusura tisa nchini Myanmar.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha