Meli kubwa ya kwanza ya utalii inayoundwa nchini China yafanya safari ya kwanza mjini Qingdao (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 07, 2025
Meli kubwa ya kwanza ya utalii inayoundwa nchini China yafanya safari ya kwanza mjini Qingdao
Watalii wakijiandaa kupanda Meli ya Utalii ya Adora Magic City kwenye Gati la Kimataifa la Meli za Kitalii la Qingdao mjini Qingdao, Mkoani Shandong, mashariki mwa China, Aprili 6, 2025 . (Xinhua/Li Ziheng)

Ikiwa ni meli kubwa ya kwanza ya utalii inayoundwa nchini China, Adora Magic City imeanza safari yake ya kwanza ya kibiashara Januari 1, 2024. Wakati huu, meli hiyo imefanya safari yake ya kwanza katika Mji wa Qingdao, Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China, ambayo ni mara ya kwanza kwa meli hiyo kuonyeshwa katika mji huo wa bandari wa China tofauti na bandari yake ya nyumbani mjini Shanghai, na itaondoka kuelekea Mji wa Jeju wa Korea Kusini na Mji wa Fukuoka wa Japan. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha