

Lugha Nyingine
Mtu aokolewa katika eneo la Nay Pyi Taw nchini Myanmar siku 5 baada ya tetemeko la ardhi (4)
YANGON - Mfanyakazi wa hoteli mwenye umri wa miaka 26 ameokolewa kutoka kwenye vifusi vya jengo la hoteli lililoporomoka mjini Nay Pyi Taw nchini Myanmar jana Jumatano, siku tano baada ya tetemeko la ardhi la ukubwa wa 7.9 kutokea katika nchi hiyo, taarifa iliyotolewa na timu ya habari ya Kamati ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mambo ya Utawala ya Myanmar imeeleza.
Timu hiyo ya habari imesema, watu wawili walikuwa wamenaswa chini ya vifusi, na timu za uokoaji kutoka Idara za Huduma za Zimamoto za Myanmar na Uturuki zimemvuta kwa mafanikio mmoja aliyenusurika kwenda mahali salama.
“Shughuli ya uokoaji kwenye hoteli hiyo ilianza majira ya saa 9:00 alasiri kwa saa za Myanmar juzi Jumanne, na mtu huyo ameokolewa saa 6:30 jioni kwa saa za huko siku ya Jumatano,” taarifa imesema.
Imeongeza kuwa, juhudi zinaendelea kutafuta na kuokoa watu waliobaki wakiwa wamenaswa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma