Waokoaji kutoka China Bara na Hong Kong washirikiana nchini Myanmar (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 02, 2025
Waokoaji kutoka China Bara na Hong Kong washirikiana nchini Myanmar
Katika picha hii, Timu ya Uokoaji ya China, iliyotumwa na Wizara ya Usimamizi wa Dharura ya nchi hiyo, na timu ya uokoaji kutoka Hong Kong ya China zinashirikiana kufanya utafutaji na uokoaji katika makazi ya Sky Villa, Mandalay, Myanmar, Aprili 1, 2025. (Xinhua/Cai Yang)

Vifaa, vikiwemo endoskopu za jicho la nyoka, kamera za mawimbi ya rada na droni, zimetumika katika kazi ya pamoja kati ya Timu ya Uokoaji ya China na timu ya uokoaji kutoka Hong Kong ya China. Kikitumia droni katika eneo la tukio, kikosi hicho cha pamoja cha uokoaji kimefanya tathmini ili kuhakikisha usalama wa uokoaji.

Awali wenyeji walitoa habari kwamba kuna sauti za kuhitaji uokoaji kwenye eneo la tukio ambapo waokoaji hao wa China walikimbilia haraka mahali hapo na baada ya juhudi walithibitisha kwamba hakuna manusura.

Waokoaji 24 walishiriki katika kazi hiyo ya pamoja. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha