

Lugha Nyingine
Habari picha: Mrithi wa sanaa ya kudarizi ya Kabila la Wahan mkoani Hubei, China
![]() |
Ren Wei akifanya kazi ya kudarizi kwenye studio yake mjini Wuhan, Mkoani Hubei, katikati mwa China, Machi 14, 2025. (Xinhua/Du Zixuan) |
Sanaa ya kudarizi ya Kabila la Wahan, udarizi wa kijadi wenye historia ya miaka zaidi ya 2,000, iliorodheshwa kama mojawapo ya vitu vya urithi wa kitaifa wa utamaduni usioshikika wa China mwaka 2008. Ikiwa maarufu kwa ufumaji wake mkali, rangi nyingi na mapambo thabiti, mara nyingi inaonyesha mapambo kwa mistari ya dhahabu au fedha, ikitoa mwonekano mzuri sana.
Ren Wei, alizaliwa katika familia ya sanaa ya kudarizi ya kabila la Wahan, ni mrithi mwakilishi wa sanaa hiyo. Tangu alipokuwa na umri wa miaka 14, Ren alikuwa akifanya kazi katika studio ya baba yake na kujifunza ustadi huo kutoka kwake.
Ili kurithisha ufundi huo vyema, Ren na baba yake wametumia makumi ya miaka kukusanya na kurejesha mitindo ya kijadi kwa kutembelea makavazi nyingi na wasanii wa asili. Kwake, sanaa inapaswa kujumushwa na maisha ya kisasa badala ya kubaki tu kwenye majumba ya makumbusho.
Tangu mwaka 2014, Ren amekuwa akifungua madarasa ya bila malipo ya ya sanaa hiyo ya kudarizi ya Kabila la Wahan kwa wanafunzi wapatao mia moja katika shule ya wanafunzi wenye tatizo la kusikia na kuona mjini Wuhan, Mkoani Hubei, katikati mwa China.
Mwaka 2015, alishirikiana na mbunifu Zhao Huizhou kuchanganya darizi hizo za kabila la Wahan na usanifu wa mitindo ya kisasa ya mavazi. Kazi zao za sanaa zimeonyeshwa kwenye Wiki ya Mitindo ya Milan, Italia. Kwa uungaji mkono wa serikali ya mtaa, pia ameunda bidhaa nyingi za kitamaduni na kibunifu, kufungua madarasa na kujenga kumbi za maonyesho ya kidijitali. Siku hizi, binti yake pia amejiunga naye katika urithi wa ustadi huo.
"Ingawa teknolojia ya AI na mbinu za uchapishaji wa 3D zimeathiri viwanda vya kazi za mikono, haziwezi kuelezea hisia na moyo wa udarizi wa kabila la Wahan." Amesema Ren Wei, akielezea matumaini yake kuwa watu zaidi wanaweza kuungana nao ili kujenga mustakabali nzuri zaidi wa sanaa hiyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma