Shehena ya kwanza ya vitu vya msaada wa China yawasili Myanmar (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 01, 2025
Shehena ya kwanza ya vitu vya msaada wa China yawasili Myanmar
Wafanyakazi wakijiandaa kusafirisha shehena ya kwanza ya vitu vya msaada uliotolewa na serikali ya China katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Yangon mjini Yangon, Myanmar, Machi 31, 2025. (Picha na Haymhan Aung/Xinhua)

ANGON – Shehena ya kwanza ya China ya vitu vya msaada wa dharura wa kibinadamu kwa Myanmar iliyokumbwa na tetemeko la ardhi imesafirishwa kutoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing jana Jumatatu asubuhi na kuwasili Myanmar siku hiyo hiyo.

Kwa kuitikia ombi la serikali ya Myanmar, China imeamua kuipatia Myanmar Yuan milioni 100 (dola za Kimarekani milioni 13.9) kama msaada wa dharura wa kibinadamu ili kuunga mkono juhudi za kukabiliana na tetemeko la ardhi.

Kwa mujibu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la China, vifaa hivyo vya msaada vya shehena ya kwanza vinajumuisha mahema, blanketi na vifaa vya huduma ya kwanza.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha