

Lugha Nyingine
Idadi ya waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi nchini Myanmar yaongezeka hadi 2,056 (5)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 01, 2025
![]() |
Wakazi walioathiriwa na tetemeko wakiwa wamepumzika msituni kando ya barabara, Nay Pyi Taw, Myanmar, Machi 31, 2025. (Picha na Wang Shen/Xinhua) |
YANGON - Idadi ya watu waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.9 kwenye kipimo cha richta lililotokea Ijumaa nchini Myanmar imeongezeka hadi kufikia watu 2,056, huku watu takriban 3,900 wakiwa wamejeruhiwa na karibu 270 wakiwa bado hawajajulikani walipo, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Timu ya Habari ya Baraza la Utawala la Nchi ya Myanmar jana Jumatatu.
Waokoaji wa ndani na nchi za nje wamekuwa wakishindana dhidi ya wakati kuokoa maisha zaidi katika maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko hilo.
Shehena ya kwanza ya vitu vya misaada iliyotolewa na serikali ya China imewasili Myanmar jana siku hiyo ya Jumatatu.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma