Hafla ya kumtambika babu shujaa Huangdi yafanyika kwa shangwe mkoani Henan, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 01, 2025
Hafla ya kumtambika babu shujaa Huangdi yafanyika kwa shangwe mkoani Henan, China
Hafla ya kumtambika Huangdi, babu shujaa maarufu wa Wachina wote wa vizazi vyote kwa pamoja, ikifanyika katika Mji wa Xinzheng, Mkoa wa Henan, katikati mwa China, Machi 31, 2025.(Xinhua/Zhu Xiang)

Watu wa China wameshiriki kwenye hafla kubwa jana Jumatatu katika Mji wa Xinzheng, Mkoa wa Henan, katikati mwa China kumwabudu babu shujaa maarufu Huangdi --Mfalme Huang ambaye ni babu wa Wachina wote wa vizazi vyote kwa pamoja.

Jana Tarehe 3 Machi kwa kalenda ya kilimo ya China, inaaminika sana kuwa ni siku ya kuzaliwa kwa Huangdi. Akiwa babu shujaa maarufu wa wachina wote wa vizazi vyote kwa pamoja, Huangdi aliaminika kuwa alizaliwa katika mji wa wilaya wa Xinzheng.

Kumtambika Huangdi ni mila na jadi nchini China. Hafla ya kumtambika Babu Huangdi katika mji huo alikozaliwa Huangdi iliwekwa kwenye orodha ya kitataifa ya China ya mali ya urithi wa kitamaduni usioshikika mwaka 2008.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha