

Lugha Nyingine
Chai ya Juyan ya Wuzhou yaingia msimu wa mavuno mkoani Zhejiang, China
Chai ya Juyan ya Wuzhou (jina la kale la Jinhua) imeingia hivi karibuni katika msimu wake wa mavuno. Mbinu ya kutengeneza chai hiyo ya Juyan, pamoja na ile ya chai ya Longjing (chai ya Kisima cha Dragoni cha Ziwa Xihu), chai ya Zisun (aina ya chai inayotoka wilaya ya Changxing) na aina zingine maarufu za chai mkoani Zhejiang, ziliorodheshwa kwenye Orodha ya Urithi wa Utamaduni Usioshikika Duniani mwaka 2022.
Katika miaka ya hivi karibuni, kwa juhudi za pamoja kutoka kwa kampuni ongozi za chai na warithi wa mbinu ya kutengeneza chai ya Juyan, chai hiyo imeongeza kasi yake ya maendeleo na kuelekea kwenye uzalishaji na maendeleo ya viwanda yaliyosanifishwa. Maendeleo ya viwanda vya kutengeneza chai ya Juyan yamekuza utalii wa kiikolojia wa kienyeji na kusaidia kuongeza mapato ya wakulima wenyeji.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma