Timu za uokoaji za China zashindana dhidi ya wakati kuokoa maisha nchini Myanmar (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 31, 2025
Timu za uokoaji za China zashindana dhidi ya wakati kuokoa maisha nchini Myanmar
Waokoaji wakijiandaa kufanya shughuli za uokoaji baada ya tetemeko la ardhi mjini Mandalay, Myanmar, Machi 30, 2025. (Picha na Myo Kyaw Soe/Xinhua)

NAY PYI TAW/MANDALAY/KUNMING - Tangu tetemeko la ardhi la kipimo cha Richta 7.9 liikumbe Myanmar siku ya Ijumaa, timu kadhaa za uokoaji za China zimewasili katika nchi hiyo ya Asia Kusini-Mashariki na zinashindana dhidi ya wakati kuokoa maisha pamoja na timu za uokoaji za nchini humo.

Timu ya watu 37 ya uokoaji na matibabu kutoka Mkoa wa Yunnan wa China imewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Yangon wa Myanmar majira ya saa 1 asubuhi kwa saa za Mynmar siku ya Jumamosi, ikiwa imebeba vifaa vya dharura kama vile vifaa vya kugundua uhai wa watu, mifumo ya tahadhari ya mapema ya tetemeko la ardhi, simu za satalaiti zinazobebeka kirahisi na droni.

Timu hiyo mara moja ilijiunga na kikosi cha zima moto na uokoaji cha Myanmar na kuelekea katika mji mkuu ulioathirika vibaya wa Nay Pyi Taw. Jumamosi jioni, timu hiyo ya uokoaji ilifika katika mji mkuu huo na kuanza kazi ya uokoaji mara moja.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha