

Lugha Nyingine
Gari la kuruka angani la XPENG lakamilisha majaribio ya usafiri katika Mkoa wa Hunan, China (2)
CHANGSHA - Gari la “Chombo cha Ardhini Kubeba Abiria Angani" (Land Aircraft Carrier,) lililoundwa na kampuni ya kuunda magari yanayotumia umeme ya China, XPENG, limekamilisha majaribio ya hadharani ya usafiri kwenye anga jana Alhamisi huko Changde, Mkoa wa Hunan, katikati mwa China.
Moduli hiyo ya gari la kuruka angani limefanya usafiri wa kuvuka ziwa. Likiruka hadi urefu wa mita 40, lilitua katika eneo la awali salama baada ya kuzunguka Ziwa Liuye, eneo la vivutio vya utalii huko Changde.
"Gari hili la kuruka angani linaweza kutumika kwa madhumuni ya utalii wa kutazama mandhari na kufanya uokoaji," amesema Zhao Deli, mwanzilishi wa shirika la Huitian chini ya kampuni ya gari la kuruka angani la XPENG.
Gari hilo la kuruka lina moduli ya ardhini na moduli ya angani. Moduli ya ardhini ni gari linalotumia nishati ya umeme wakati moduli ya angani inajulikana kama gari linalotumia nishati ya umeme la kupaa na kutua kwa wima (eVTOL).
Mwaka jana, majaribio ya usafiri angari yalifanyika Lujiazui, Shanghai. Bidhaa hiyo tayari imepokea oda karibu 5,000.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma