Naibu Waziri Mkuu wa China atoa wito wa kulinda biashara huria kwenye mkutano wa mwaka wa Boao

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 28, 2025
Naibu Waziri Mkuu wa China atoa wito wa kulinda biashara huria kwenye mkutano wa mwaka wa Boao
Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akihutubia ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka 2025 wa Baraza la Asia la Boao mjini Boao, Mkoani Hainan, kusini mwa China, Machi 27, 2025. (Xinhua/Yao Dawei)

BOAO, Hainan- Mkutano wa Mwaka 2025 wa Baraza la Asia la Boao (BFA) umefunguliwa jana Alhamisi mjini Boao, Mkoani Hainan, kusini mwa China ambapo Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang, alihudhuria ufunguzi wa mkutano huo, akitoa wito wa kuimarisha hali ya kuaminiana, kuboresha ushirikiano wa kunufaishana, kuhimiza utandawazi wa kibiashara na kulinda mfumo wa biashara huria.

Likiwa lilianzishwa mwaka 2001, BFA ni shirika lisilo la kiserikali na lisilo la faida la kimataifa lenye dhamira ya kuhimiza mafungamano ya kiuchumi ya kikanda na kuleta nchi za Asia karibu zaidi na malengo yao ya maendeleo. Ukiwa umepangwa kufanyika kuanzia Machi 25 hadi leo Ijumaa, Machi 28, mkutano wa mwaka huu una kaulimbiu ya "Asia katika Dunia Inayobadilika: Kuelekea Mustakabali wa Pamoja."

Akihutubia ufunguzi wa mkutano huo, Ding ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema kuwa maendeleo makubwa yamepatikana katika kujenga jumuiya ya Asia yenye mustakabali wa pamoja katika muongo mmoja uliopita.

"China na ASEAN zimeanzisha ushirikiano wa kimkakati wa pande zote, na Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Pande Zote wa Kikanda umeanza kutekelezwa," naibu waziri mkamu huyo amesema, akiongeza kuwa mafungamano ya kiuchumi kikanda yameimarishwa zaidi, na sehemu ya Asia katika uchumi wa dunia inaongezeka kwa kasi.

"Dunia yetu inakabiliwa na kuongezeka kwa ukosefu wa utulivu na kutokuwa na uhakika," Ding amesema, akitoa wito wa juhudi za pamoja kushughulikia changamoto za kimataifa, kujenga maskani ya pamoja ya Asia na kujenga mustakabali mzuri zaidiwa Asia na dunia.

Ni muhimu kuimarisha mshikamano na ushirikiano kupitia kuongeza hali ya kuaminiana, Ding amesema, huku akiongeza kuwa juhudi zinapaswa kufanywa ili kutetea maadili ya Asia ya amani, ushirikiano, ujumuishaji na mafungamano, na kuheshimu maslahi ya kimsingi na masuala makuu yanayofuatiliwa na kila upande.

Ding amesisitiza umuhimu wa kuhimiza utandawazi wa kiuchumi kupitia uwazi na mafungamano, akihimiza juhudi za kulinda kwa pamoja mfumo wa biashara huria, kushikilia ukanda wenye uwazi, na kupinga kithabiti kujihami kibiashara na kiuwekezaji.

Amesisitiza haja ya kulinda utulivu kupitia kuishi pamoja kwa amani. "Maono ya usalama wa pamoja, wa pande zote, wa kiushirikiano na ulio endelevu barani Asia yanapaswa kudumishwa, wakati huohuo juhudi zinapaswa kufanywa ili kuhakikisha kuwa Asia inaendelea kuwa ardhi ya amani na utulivu," Ding amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha