

Lugha Nyingine
Wilaya ya Nanhu ya Mkoa wa Zhejiang, China yaendeleza maendeleo bora ya sekta binafsi (6)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 28, 2025
![]() |
Wafanyakazi wakiunganisha sehemu za zana za bustani kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi kwenye karakana ya Kampuni ya Vifaa vya Umme ya Zhejiang Yat katika Mji wa Yuxin, Wilaya ya Nanhu mjini Jiaxing, Mkoani Zhejiang, mashariki mwa China, tarehe 26 Machi 2025. (Xinhua/Xu Yu) |
Wilaya ya Nanhu ya mji wa Jiaxing katika Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China imekuwa ikijikita katika kuendeleza maendeleo bora ya sekta binafsi na kuchochea uhai wa soko kwa kutumia sera nafuu na kuanzisha miradi mipya katika miaka ya hivi karibuni.
Mwaka 2024, wilaya hiyo ilianzisha utaratibu wa kivumbuzi ambao uliboresha sana mazingira ya biashara kwa kurahisisha mchakato wa mambo husika.
Kulikuwa na miradi mikubwa 20 ya viwanda kama vile vifaa vya kisasa na nyenzo mpya za hali ya juu zilizozalishwa kwa mara ya kwanza wilayani humo mwaka 2024, na miradi mipya 65 inayoendelea kujengwa kwa kasi, ikileta ongezeko la asilimia 15 ya uwekezaji katika sekta ya uzalishaji wa viwanda.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma