Eneo la Jimo la Mji Qingdao, China lahimiza maendeleo endelevu ya sifa bora ya viwanda vya ufumaji na utengenezaji wa nguo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 27, 2025
Eneo la Jimo la Mji Qingdao, China lahimiza maendeleo endelevu ya sifa bora ya viwanda vya ufumaji na utengenezaji wa nguo
Mfanyakazi wa kiwanda cha nguo katika eneo maalum la viwanda akitoa mafunzo kwa wafanyakazi kuhusu vifaa na ujuzi mpya katika Eneo la Jimo la Mji Qingdao, Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China, Machi 25, 2025.

Eneo la Jimo la Mji wa Qingdao, China limekuwa likiongoza hatua kwa hatua viwanda binafsi kuongeza Utafiti na Maendeleo ya Uzalishaji Bidhaa Mpya (R&D) na uwekezaji katika teknolojia mpya, vifaa vipya na teknolojia mpya za uchakataji katika miaka ya karibuni.

Wakati huo huo, pamoja na hatua za kukidhi mahitaji ya nafasi za ajira ya viwanda na kutoa mafunzo ya ujuzi kwa wafanyakazi , maendeleo endelevu ya sifa bora ya viwanda vya ufumaji na utengenezaji wa nguo yamekuwa yakihimizwa ipasavyo, na wakazi wengi wa huko wameajiriwa na kushuhudia mapato yao yakiongezeka.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha