

Lugha Nyingine
Boao, China yaanzisha eneo la utoaji kaboni-sifuri ili kutafuta maendeleo endelevu
![]() |
Picha hii iliyopigwa Machi 25, 2025 ikionyesha eneo la msitu wa minazi katika eneo la kielelezo la utoaji kaboni-sifuri la Boao, Mkoani Hainan, kusini mwa China. (Xinhua/Yang Guanyu) |
BOAO, Hainan – Kijiji cha Boao cha China kimetangaza kuanzisha eneo la kwanza la utoaji kaboni-sifuri, ikiwa ni maendeleo makubwa katika jitihada za nchi hiyo za kupunguza utoaji wa kaboni, serikali ya Mkoa wa Hainan imeeleza.
Mtaalamu mmoja amesema kuwa mafanikio hayo ni mfano tangulizi kwa juhudi za kimataifa za kupunguza kaboni, na yanasisitiza dhamira ya China ya usawazishaji kaboni na maendeleo endelevu.
Likichukua eneo lenye ukubwa wa hekta takriba 190, eneo hilo la kielelezo linajumuisha Kisiwa cha Dongyu, ambacho ni eneo la kudumu la mkutano wa kila mwaka wa Baraza la Asia la Boao (BFA).
Kwa kujikita katika ukarabati wa ujenzi wa kijani na matumizi ya nishati mbadala, eneo hilo la kielelezo limefanikiwa kupunguza utoaji kaboni dioksidi kwenye majengo na miundombinu mingine kutoka tani 11,300 mwaka 2019 hadi tani sifuri mwaka 2024, kwa mujibu wa takwimu kutoka serikali ya mkoa.
Tangu kuzinduliwa kwake rasmi mwaka 2001, BFA imekuwa ikitumika kama jukwaa muhimu la kuendeleza maendeleo ya kijani kote Asia, likiwezesha mawasiliano ya maarifa ili kuhimiza ukuaji endelevu katika kanda na kwingineko.
Bara la Asia linasonga mbele kwa kasi katika teknolojia inayoibukia ya kijani, ikijiweka kama kiongozi tarajiwa katika nyanja kama vile vifaa vya hali ya juu vya betri na plastiki inayoweza kuoza, ikitokana na uwezo wake mkubwa wa kiviwanda na uungaji mkono wa kisera, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa jana Jumanne na BFA.
China iko katika mstari wa mbele wa sekta ya hidrojeni ya kijani ya Asia inayopanuka na sasa inapata asilimia 85 ya uwezo wake mpya wa nishati kutoka nishati mbadala, ripoti hiyo imeeleza.
Nchi zinazotoa hewa chafuzi nyingi zaidi za Asia, ikiwemo China, zimeweka malengo makubwa ya tabianchi, ripoti hiyo inasema. Inasema kuwa kwa mujibu wa Shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa, China na India zimetathminiwa kuwa na uwezekano wa kufikia malengo yao ya sasa ya Mchango ulioamuliwa Kitaifa wa 2030 kwa sera zao zilizopo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma