Wilaya ya Kabila la Watajik ya Taxkorgan, Xinjiang, China yatumia urithi wa kitamaduni kukuza utalii (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 25, 2025
Wilaya ya Kabila la Watajik ya Taxkorgan, Xinjiang, China yatumia urithi wa kitamaduni kukuza utalii
Magari yakionekana kwenye eneo la kivutio cha watalii lenye barabara za mizunguko baada ya kufunguliwa kwake kwa umma katika Wilaya inayojiendesha ya Kabila la Watajik ya Taxkorgan, Mkoani Xinjiang, kaskazini-magharibi mwa China, Machi 22, 2025. (Xinhua/Hu Huhu)

Wilaya inayojiendesha ya Kabila la Watajik ya Taxkorgan, Mkoani Xinjiang unajivunia urithi mbalimbali wa kitamaduni usioshikika.

Katika wakati huu wa kipindi cha mlingano wa usiku na mchana wa Majira ya Mchipuko, ambacho ni kipindi cha nne cha mzunguko wa jua katika kalenda ya kilimo ya China, ambacho kiliangukia Machi 20 mwaka huu, wilaya hiyo imekuwa ikifungamanisha rasilimali zake za mazingira na utamaduni wake wa jadi wa kikabila kufanya maonyesho ya urithi wa kitamaduni usioshikika na shughuli za kitamaduni na michezo, kama njia ya kuvutia watalii na kutangaza utalii wake katika majira ya mchipuko.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha