Kampuni ya China ya kutengeneza saa, SEA-GULL yasherehekea mwaka wa 70 tangu kutengeneza saa ya kwanza

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 25, 2025
Kampuni ya China ya kutengeneza saa, SEA-GULL yasherehekea mwaka wa 70 tangu kutengeneza saa ya kwanza
Picha hii iliyopigwa Machi 24, 2025 ikionyesha saa ya kwanza kutengenezwa nchini China ikionyeshwa kwenye jumba la makumbusho la kampuni ya kutengeneza saa, SEA-GULL mjini Tianjin, kaskazini mwa China. (Xinhua/Zhao Zishuo)

TIANJIN – Jana Jumatatu, SEA-GULL, kampuni ya kutengeneza saa yenye makao yake makuu katika Mji wa Tianjin kaskazini mwa China, imefanya shughuli mbalimbali za maadhimisho ya kutimia miaka 70 tangu kutengenezwa kwa saa ya kwanza ya nchi ya China Mpya.

Mwaka 1955, saa hiyo ilitengenezwa kwa mafanikio mjini Tianjin, ikionesha SEA-GULL kuwa mahali pa kuzaliwa kwa saa hiyo ya kwanza ya China yenye kutukuka kwa muda mrefu.

Baada ya miongo saba ya juhudi za utafiti na maendeleo, kampuni hiyo sasa imebobea katika teknolojia ya hali ya juu ya kutengeneza saa yenye hakimiliki ya ubunifu kwa kujitegemea.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha