

Lugha Nyingine
Maandhari ya Kijiji cha Kabila la Wadong cha Zhaoxing mkoani Guizhou, China
Kikiwa kinapatikana katika Wilaya ya Liping ya Eneo linalojiendesha la Makabila ya Wamiao na Wadong la Qiandongnan, Mkoa wa Guizhou, kusini-magharibi mwa China, Kijiji cha Kabila la Wadong cha Zhaoxing ni maskani ya kaya zaidi ya elfu moja za watu wa kabila la Wadong. Mtindo wa jadi wa usanifu majengo na urithi tajiri wa kitamaduni wa kabila hilo la Wadong vimehifadhiwa vizuri.
Katika miaka ya hivi karibuni, huku ikidumisha uadilifu wa kihistoria wa kijiji hicho na kurithi sifa za kipekee za kitamaduni, jumuiya ya wenyeji imeanzisha timu za wimbo mkuu wa kabila la Wadong na vikundi vya opera ya kabila hilo. Sherehe za kijadi za kabila hilo zimegeuzwa kuwa vivutio vya utalii. Aidha, maendeleo ya biashara za kazi za mikono za kijadi na hoteli, nyumba za wageni, na mikahawa zaidi 433 yametoa ajira zaidi ya 2,000 kwa wanavijiji wenyeji, ikiwawezesha kupata faida za kiuchumi kutokana na sekta ya utalii.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma