

Lugha Nyingine
Biancheng: "Mji wa Mpakani" unaounganisha Hunan, Guizhou na Chongqing nchini China (4)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 20, 2025
XIANGXI - Mji wa Biancheng wa Wilaya ya Huayuan, Eneo linalojiendesha la Makabila ya Watujia na Wamiao la Xiangxi, Mkoa wa Hunan, katikati mwa China, rejelea ya mfano kwenye kazi bora ya fasihi ya mwandishi wa China Shen Congwen "Border Town", unapatikana kwenye makutano ya mikoa ya Hunan, Guizhou na Manispaa ya Chongqing nchini China.
Katika kila siku ya soko, sehemu ya soko la mji huo hujaa wakazi kutoka maeneo ya jirani, wakifanya manunuzi ya mboga mboga na mahitaji muhimu ya kila siku. Wakati huo huo, mila na mtindo wa kipekee wa watu wa kabila la Wamiao katika eneo hilo pia vimekuwa vikivutia watalii wengi.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma