Rais Xi Jinping wa China akagua Mkoa wa Guizhou na kusisitiza maendeleo ya sifa bora ya juu (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 19, 2025
Rais Xi Jinping wa China akagua Mkoa wa Guizhou na kusisitiza maendeleo ya sifa bora ya juu
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akizungumza na wanakijiji wakati wa kutembelea Kijiji cha Kabila la Wadong cha Zhaoxing, Wilaya ya Liping ya Eneo linalojiendesha la Makabila ya Wamiao na Wadong la Qiandongnan, Mkoa wa Guizhou, kusini-magharibi mwa China, Machi 17, 2025. (Xinhua/Yan Yan)

GUIYANG - Rais wa China Xi Jinping amesisitiza umuhimu wa kutilia maanani maendeleo ya sifa bora ya juu na kuhimiza ukuaji wa uchumi kwa kuimarisha mageuzi na ufunguaji mlango kwa kina, wakati wa ziara yake ya ukaguzi katika Mkoa wa Guizhou, kusini magharibi mwa China iliyofanyika kuanzia Jumatatu hadi Jumanne wiki hii.

Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ametoa wito kwa mkoa huo kuimarisha imani yao, kufanya kazi kwa bidii, na kuchukua hatua madhubuti ili kuendeleza ujenzi wa mambo ya kisasa wa China.

Siku ya Jumatatu mchana, Rais Xi alitembelea Kijiji cha kabila la Wadong katika Eneo linalojiendesha la makabila ya Wamiao na Wadong la Qiandongnan. Alikagua hali halisi ya mazingira na maduka ya wenyeji, akisimama mara kwa mara ili kuongea na wamiliki wa maduka hayo, watalii, na wanakijiji.

Amesisitiza kwamba tamaduni za makabila madogo mbalimbali ni sehemu muhimu ya utamaduni wa China na zinapaswa kuhifadhiwa, vilevile ni lazima kufanya ubunifu wa aina mpya ili utamaduni wa makabila madogo mbalimbali kuwa na sura mpya ya kung’aa.

Rais huyo wa China pia aliketi na wanakijiji kwa mazungumzo, ambapo alielezea matumaini yake kwamba wanaweza kustawisha zaidi kijiji katika wakati wa ujenzi wa mambo ya kisasa wa China.

Rais Xi pia alitembelea mji mkuu wa mkoa huo, Guiyang jana Jumanne, ambapo alisikiliza ripoti za kazi zilizotolewa na serikali ya mkoa na kamati ya chama ya mkoa huo.

Amesisitiza kuimarisha maendeleo yanayohimizwa kwa uvumbuzi huku uchumi halisi ukiwa msingi. Ametoa wito wa kuendeleza kikamilifu viwanda vya kimkakati vinavyoibuka na kuimarisha uchumi wa kidijitali na kazi za nishati mpya.

Pia ameutaka mkoa huo kulinda mazingira vizuri na kubadilisha nguvu bora zake za kiikolojia kuwa nguvu bora ya kujipatia maendeleo.

Rais Xi amesisitiza haja ya kuendeleza kilimo cha kisasa, chenye ufanisi na chenye sifa bainifu za sehemu ya milimani kwa kufuata mazingira halisi ya mkoa huo wa Guizhou, huku ukijenga na kukuza shughuli zenye umaalum wa kimkoa na kuwa na nguvu ya ushindani wa kudumu sokoni.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha