Mashamba makubwa ya miti ya cherry yachanua kwa wingi Guizhou, China (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 14, 2025
Mashamba makubwa ya miti ya cherry yachanua kwa wingi Guizhou, China
(Tu Min/People’s Daily Online)

China kwa sasa iko katika msimu wa uamsho kwa maana ya kuamka, kuota na kustawi tena kwa viumbe hai, na mashamba makubwa ya miti ya cherry katika kijiji cha Aohe, mkoa wa Guizhou wa nchi hiyo yamechanua kwa wingi.

Kijiji hicho cha Aohe kina mandhari ya kuvutia ya milima mikubwa na miteremko mikali. Wanakijiji wa Aohe walianza kupanda miti ya cherry kuanzia mwaka 2014. Wakati maua ya miti hiyo ya cherry yanapochanua, huvutia watalii kuja kufurahia mandhari ya maua na kufanya matembezi ya nje. Wakati matunda hayo ya cherry yanapokomaa na kuiva huchumwa na kuonjwa yakiwa freshi. Mashamba hayo ya cherry yamekuwa chanzo muhimu kwa wakazi wenyeji kuongeza kipato chao.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha