

Lugha Nyingine
Majaji wanawake watekeleza majukumu yao ya kila siku mjini Beijing, China
![]() |
Hou Yanrong (kulia), jaji katika Mahakama ya Umma ya Eneo la Haidian la Beijing, akiendesha kesi mtandaoni katika Mahakama mjini Beijing, Machi 6, 2025. (Xinhua/Huang Bohan) |
Jana Tarehe 10 Machi ilikuwa ni Siku ya Majaji Wanawake Duniani, ambayo iliwekwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Mwaka 2021 ili kusisitiza mchango wa wanawake katika mfumo wa mahakama na kuwatia moyo wanawake zaidi kutekeleza majukumu ya kimahakama.
Kabla ya Siku hiyo, waandishi wa habari wa Shirika la Habari la China, Xinhua walitembelea majaji wanawake wa Mahakama ya Umma ya Eneo la Haidian la Beijing. Majaji hao wanawake wanashiriki kwa umakini katika huduma za ofisini na nje ya ofisi kama vile kufungua kesi na mambo ya mashtaka, hukumu za kesi mahakamani, kusuluhisha migogoro, kusimamia utekelezaji wa uamuzi wa mahakama, na kampeni za habari za kujenga uelewa wa umma.
Kwa hekima na bidii yao, majaji hao wanawake wanaheshimu uhalali wa mahakama za kisheria, na kulinda haki na usawa kwa jamii.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma