

Lugha Nyingine
Mjumbe wa Bunge la Umma la China atoa wito wa kusukuma maendeleo kwa uvumbuzi katika tasnia ya magari (2)
Feng Xingya, mwenyekiti wa kundi la kampuni za kuunda magari la China, GAC, amekuwa akifanya kazi katika tasnia ya magari kwa miaka zaidi ya 30. Ameshuhudia maendeleo ya tasnia ya magari ya China. Akiwa mjumbe wa Bunge la 14 la China, Feng hutilia maanani sana kufanya utafiti na uchunguzi kwenye mahali pa kuzalisha magari.
Kabla ya mkutano wa tatu wa Bunge hilo la 14 unaoendelea mjini Beijing, Feng alikuwa punde amemaliza ziara ya ukaguzi nchini Uturuki na kufanya utafiti wa soko la ndani mjini Beijing.
Feng amesema, katika kukabiliana na mageuzi katika tasnia ya magari duniani, uvumbuzi lazima uwe nguvu endeshi. Amesisitiza haja ya kuimarisha uwezo wa kuvumbua kwa kujitegemea katika kupata mafanikio mapya kwenye teknolojia muhimu na kuanzisha mfumo wa ikolojia ya kiviwanda ulio salama na thabiti.
Kwenye mkutano huo wa mwaka huu wa Bunge hilo, Feng amewasilisha mapendekezo juu ya kushughulikia changamoto muhimu katika tasnia ya magari yanayotumia nishati mpya ya China (NEV).
Pia anatoa wito wa uungwaji mkono wa sera na mbinu fanisi za soko ili kusongesha mbele sekta ya NEV ya nchi hiyo kuelekea maendeleo ya kijani, mahiri na endelevu zaidi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma