

Lugha Nyingine
Canada yatangaza kifurushi cha ushuru wa kulipiza dhidi ya Marekani chenye mlolongo wa bidhaa (4)
![]() |
Mwanamke akitembea kulipita bango lenye maneno "PROUDLY CANADIAN" kwenye supamaketi mjini Toronto, Ontario, Canada, Machi 4, 2025. (Picha na Zou Zheng/Xinhua) |
OTTAWA - Serikali Kuu ya Canada imetangaza kifurushi cha ushuru chenye mlolongo wa bidhaa baada ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo Justin Trudeau kuapa kwamba Canada haitarudi nyuma kutoka kwenye mapambabno dhidi ya vita vya kibiashara vilivyoanzishwa na Rais wa Marekani Donald Trump.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Wizara ya Fedha ya Canada jana Jumanne, awamu ya kwanza ya mwitikio wa Canada inajumuisha ushuru wa dola za Canada bilioni 30 (dola za Kimarekani karibu bilioni 21) kwa bidhaa za kuagizwa kutoka Marekani, mara moja, kuanzia saa 6:01 usiku, Machi 4.
Orodha hiyo inajumuisha bidhaa kama vile juisi ya machungwa, siagi ya karanga, divai, vinywaji vikali, bia, kahawa, vifaa, mavazi, viatu, pikipiki, vipodozi, na baadhi ya bidhaa za mbao na karatasi.
Hatua za ziada za kulipiza za kutoza dola bilioni 125 za Canada (dola za Kimarekani kama bilioni 89) kwenye bidhaa za kuagizwa kutoka Marekani zitatoka kwenye orodha ya bidhaa zilizo wazi kwa muda wa siku 21 wa maoni ambazo zinajumuisha bidhaa kama vile magari yanayotumia umeme, matunda na mboga za majani, nyama ya ng'ombe, ya nguruwe, bidhaa za maziwa, vifaa vya elektroniki, chuma, aluminiamu, malori, na mabasi, taarifa hiyo imeeleza.
“Serikali pia inachukua hatua za kupunguza athari za hatua hizi za kulipiza kwa wafanyakazi na wafanyabiashara wa Canada kwa kuanzisha mchakato wa msamaha kufikiria maombi ya unafuu maalum kutoka kwa ushuru,” taarifa hiyo inasema.
Imesema kuwa, machaguo yote yanabakia kuwa mezani wakati ambapo serikali ya nchi hiyo inafikiria hatua za ziada, ikiwemo machaguo ya hatua zisizo za kiushuru.
Trudeau amesema katika hotuba yake kwa taifa mapema siku hiyo kwamba Canada pia itapinga hatua hizo haramu za Marekani kwa kuwasilisha madai ya utatuzi wa migogoro katika Shirika la Biashara Duniani na kupitia Makubaliano ya Canada-Mareknai-Mexico, au utaratibu wa biashara huria wa Amerika Kaskazini ambao ulijadiliwa na kurekebishwa masharti yake tena na Trump katika muhula wake wa kwanza wa urais.
“Ushuru huo wa kulipiza utaendelea kubaki hadi ushuru huo wa Marekani utakapoondolewa na siyo muda mfupi,” Trudeau amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma